COSTECH YATOA MAFUNZO KUHUSU UWASILISHAJI WA HABARI ZA KISAYANSI KWA WATAFITI NA WAANDISHI WA HABARI - KANDA YA MASHARIKI

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imewakutanisha kwenye mafunzo waandishi wa habari na watafiti kutoka kanda ya mashariki ili kuwajengea uwezo wa kufikisha matokeo ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kwa walengwa. Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo ya siku mbili, kaimu Mkurugenzi wa idara ya Menejimenti ya Maarifa ndugu Emmanuel Nnko ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu. Ndugu Nnko amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa jitihada za Tume za kuhakikisha tafiti zinazofanywa nchini zinawafiia walengwa na kuleta tija kwa jamii.

Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi za utafiti wa mifugo Tanzania (TALIRI) Dkt. Zabron Nziku amesema matokeo ya utafiti ndiyo yanayoweza kusaidia uchumi wa viwanda endapo yatawafikia walengwa na kuyatumia. Amesema kuwa tafiti nyingi zinafanywa lakini zinaishia kwenye vituo vya utafiti na hivyo wananchi na wadau wa tafiti hizo kutonufaika nazo wakati zimetumia fedha nyingi.

Katika ufunguzi Kaimu Mkurugenzi wa TARILI pia amepongeza programu hiyo ambayo inafanywa na COSTECH nchi nzima na kuwataka waandishi wa habari kuyafanyia kazi ili yaweze kusaidia jamii ya Watanzania.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo, Dkt. Zabron Nziku, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwani yanasaidia kuwaleta pamoja wanasayansi na waandishi wa habari na kupanga mikakati ya namna wanavyoweza kushirikiana katika kusaidia jamii na Taifa kwa kubuni njia bora za kuwafikishia wadau matokeo ya tafiti hizo. Aliendelea kusema kuwa, mafunzo hayo ni sehemu ya mafunzo kwa waandishi wa habari na watafiti ambayo yanafanyika nchi nzima ili kusaidia kufikia malengo ya kupata taarifa za tafiti mbalimbali zinazofanyika nchi nzima kwenye vituo na taasisi za tafiti.

Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo Afisa programu ya mafunzo hayo kutoka COSTECH ndugu Merchades Rutechura amesema ni kupunguza mipaka kati ya watafiti na waandishi wa habari nchini. Amesema kuwa toka mafunzo hayo yaanze kwenye kanda mbalimbali kumekuwa na ongezeko kubwa la Makala,vipindi na habari za Sayansi,teknolojia na Ubunifu na hivyo kusaidia jamii kujua ni wapi wanaweza kuzipata ili kuzitumia kwenye shughuli zao mbalimbali za uzalishaji na kuongeza tija. Ndugu Method aliwataka waandishi ho ambao wanawakilisha Mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Tanga kutumia kusanyiko hilo kujua miiko ya utoaji wa taarifa na kujenga mashirikiano na watafiti ili kuweza kuwatumia katika uandaaji wa vipindi vyao vinavyohusu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU).

Akiwasilisha mada kuhusu Utafiti na umuhimu wa kutoa matokeo ya utafiti Afisa Utafiti Mkuu kiongozi anayeshughulikia Makala na Machapisho kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi, amesema waandishi wa habari wana umuhimu mkubwa katika kufanyakazi hiyo kwakuwa wanasikilizwa na kuaminiwa na jamii. Dkt. Msangi aliendelea kusema katika kazi yoyote kuna miiko na maadili yake hivyo waandishi wa habari nao ni lazima wajue miiko na maadili ya kuandika habari na kuandaa vipindi vya Kisayansi na ubunifu ili waweze kufanya kazi hiyo vizuri kwa maslahi ya taifa bila kuleta matatizo kwa mtafiti na mwandishi mwenyewe. Amesisitiza wa kusema kuwa, habari za kisayansi zinahitaji ubunifu kwenye kupeleka kwa walengwa kwa kuandika habari zenye lugha nyepesi, Ufupi na kwa kutumia njia ambayo inaweza kuwafikia walengwa katika eneo fulani iwe redio,Televisheni au magazeti na hata mitandao ya ijamii.

Akimalizia kutoa mada yake, Dkt. Msangi amesema kuwa mbali na kuwafikia wakulima na wafugaji lakini pia inasaidia kuwafikia watoa maamuzi katika sekta mbalimbali nchini ili waweze kufanya maamuzi kutokana na okeo ya tafiti zilizofanyika.


 

                           Baadhi ya  washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada zinazowasilishwa.