Latest updates

COSTECH Yashiriki Uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Utafiti Kuhusu Mazingira

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeshiriki warsha ya kuhuisha Ajenda ya Taifa ya Utafiti wa Mazingira (NERA), inayosimamiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia Kamati ya Ushauri wa Utafiti kuhusu Mazingira (ERAC).

Warsha hiyo imefanyika katika Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro kuanzia tarehe 7 -8 Oktoba, 2020 ambapo washiriki wa Warsha hiyo ni wajumbe wa kamati kutoka katika Vyuo Vikuu, Sekta binafsi, Tawala za Mikoa na Taasisi mbalimbali zinazohusika na mazingira kutoka Tanzania Bara na Visiwani ambapo COSTECH ni mjumbe wa kamati hiyo.

Lengo la warsha hiyo ni kuzindua Kamati ya Ushauri wa Tafiti zinazohusu Mazingira pamoja na kuwapitisha wajumbe hao katika Ajenda ya Taifa ya Utafiti wa Mazingira 2017 – 2022 ili waweze kuifanyia maboresho.

Katika warsha hiyo, COSTECH iliwakilishwa na Bwana Merchades Rutechura ambaye aliwasilisha mada kuhusu “Nafasi ya Tume katika kuratibu na kuhamasisha tafiti zinazohusu Mazingira.”

Aidha, katika mawasilisho hayo, COSTECH iliainisha miradi ya utafiti na ubunifu iliyowahi kufadhiliwa kwa kipindi kilichoanzia mwaka 2015 – 2020; mafanikio yaliyopatikana; changamoto zinazoikumba Tume katika kuratibu na kuhamasisha tafiti zinazohusu Mazingira pamoja na njia inazotumia kutatua changamoto hizo.

Vilevile warsha hiyo iliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti wa ERAC ambapo Bw. Thomas Bwana kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira alichaguliwa kuongoza Kamati kwa kipindi cha miaka mitatu (3).

Warsha ilifunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Mhandisi Samuel Gwamaka Mafwenga.

Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Utafiti kuhusu  Mazingira kutoka Vyuo Vikuu, Sekta binafsi, Tawala za Mikoa na Taasisi  mbalimbali zinazohusika na mazingira kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Learn More

Watafiti Waahidi Kukamilisha Miongozo ya Kamati za Kusimamia Maadili ya Tafiti Katika Taasisi Zao

Watafiti kutoka katika Taasisi za tafiti nchini ambazo ni Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Taasisi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) waahidi kukamilisha miongozo ya kamati za kusimamia maadili ya utafiti katika taasisi zao.

Watafiti hao wameyasema hayo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu alipokuwa akifungua kikao Kazi cha kuandaa miongozo ya Kamati za kusimamia maadili ya Utafiti. Kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo na kimeandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) chini ya Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP).

Akifungua kikao kazi hicho Dkt. A. Nungu alisema anatamani ifikapo mwezi wa Novemba mwaka huu wa 2020 amualike Waziri kwaajili ya kuzindua miongozo yetu kutoka katika taasisi zetu za utafiti ambazo ni TALIRI, TARI, TAFORI na TAFIRI.

Dkt. Nungu alisema, COSTECH inajitahidi kujenga uwezo katika taasisi za tafiti ili ziweze kusaidia kufanya kazi kwa urahisi zaidi.

Aidha kikao kazi hiki kina jumla ya wawakilishi kumi na sita (16) kutoka katika taasisi nne ambazo kila taasisi ilileta wawakilishi wanne (4) ili kushiriki kwa pamoja katika kikao kazi hicho cha kutengeneza miongozo ya kamati za kusimamia maadili ya utafiti.

Lengo la kikao kazi  hiki ni kuwajengea uwezo Taasisi zinazojishughulisha na tafiti nchini ili ziweze kufuata taratibu na kuzingatia miongozo ya kamati za maadili ya utafiti na hatimaye kutumia matokeo ya tafiti kujibu changamoto zinazojitokeza katika jamii yetu.

Washiriki mbalimbali walieleza jinsi wanavyotekeleza majukumu yao kisheria na kuonesha uhitaji wa kupata miongozo (Standard Operating Procedure) zitakazowaongoza ili kufanikisha shughuli za utafiti na kutengeneza kamati za maadili ya kusimamia utafiti katika Taasisi zao.

Dkt. Nungu aliwapongeza kwa Kazi nzuri inayoendelea kufanywa na wadau huku akisisitiza jukumu la kimsingi la utoaji wa vibali na kuwatakia kikao kazi chema chenye mafanikio.


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha kuandaa Miongozo ya kamati za kuasimamia maadili ya utafiti yaliofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Maendeleo Uongozi wa Elimu (ADEM) – Bagamoyo.  Learn More

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Kufanya Maboresho ya Mfumo wa Kusimamia Tafiti na Bunifu

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu amesisitiza ushiriki wa pamoja kwa wataalamu wa ndani na kusema kwamba hiyo itasaidia kuboresha mfumo.

Hayo aliyasema wakati akifungua Kikao cha Kikosikazi cha Maboresho ya Mfumo wa kielektroniki wa  Utafiti na Ubunifu jana katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo iliyoko Mikocheni (MARI),  jijini Dar es Salaam.

Dkt. Nungu alisema kutokana na hilo hawana budi kujitahidi kwenda na wakati ili wanapomaliza maboresho ya mfumo wao kusitokee matatizo ya kimfumo hapo baadaye.

Akielezea katika kikao hicho Meneja wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Ndugu Emmanuel Nnko amesema tupo katika jitihada za maboresho ya mfumo wa ndani ambao utasaidia kuiwezesha Tume kusimamia na kudhibiti utaratibu mzima wa utafiti na ubunifu katika maeneo mawili, kwanza ni kutoa vibali vya miradi ya utafiti na pili kutoa ufadhili kwa wabunifu.

Vilevile amesema kwasasa wataalamu wapo katika sehemu ya awali ya ukusanyaji wa mahitaji kutoka kwa watumiaji ili kuhakikisha mahitaji yote yanaingizwa kwenye mfumo na sehemu ya pili ni maendeleo ya mfumo ya kufanikisha mahitaji hayo.

Katika Kikao hicho washiriki walioshiriki mpaka sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Wakurugenzi wa Idara mbalimbali ikiwemo Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia (CDTT), Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP) na Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa (DKM) pamoja na wadau kutoka taasisi nyingine kama TANESCO na NIDA ili kufanya maboresho ya Mfumo wa Tafiti na Ubunifu.

                             Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na wataalamu kutoka NIDA katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha kuboresha mfumo wa kusimamia Tafiti na bunifu


Learn More

Call for Proposals: Grants for Regional Innovation Projects

The Southern Africa Innovation Support Programme (SAIS 2) Innovation fund is inviting project proposals for funding through the RE:innovation challenge competition. RE:innovation is a challenge inspired by recent events.

Deadline for application is: 27th September, 2020 at 23:59 CAT

For more infomation about the call please click here

Learn More

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Yatoa Mafunzo Kuhusu COSTECH kwa Wajumbe Wapya wa Bodi

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetoa mafunzo kwa Wajumbe wapya wa Bodi kuhusu  Tume (COSTECH). 

Mafunzo hayo yalitolewa hivi karibuni katika ukumbi mdogo wa COSTECH, yalifunguliwa na Mkurugegenzi wa COSTECH Dkt. Amos Nungu.

Dkt. Nungu aliwakaribisha wajumbe wapya wa Bodi na baadaye kuwakaribisha wakuu wa idara ili kuweza kuwapitisha kwa ufupi wajumbe hao wapya ili waweze kuelewa majukumu ya Tume kwa ujumla. 

Akielezea muhtasari wa COSTECH Kaimu Meneja Kitengo cha Huduma za Sheria Bw. Ernest Barulo alisema,  Shughuli   zaTume  ya  Taifaya  Sayansi  naTeknolojia  zilianzishwa  rasmimwaka  1972 chini  yaBaraza la ufafiti (Tanzania National Scientific Research Council)  kwa kifupiUTAFITI,  lakini  mwaka1988 lilibadilishwa  kuwa  Tumeya  Taifa ya  Sayansina Teknolojia  kwa  kifupi (COSTECH)  kwamujibu wa   sheria   Na.7ya bunge   ya mwaka  1986.

Bw. Barulo alisema majukumu   Makuu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ni pamoja na kuishauri Serikali kuhusu mambo yote yanayohusu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na matumizi yake katika maendeleo Kiuchumi na Kijamii nchini.

Aidha sekretariati inasimamia utendaji wake wa kila siku wa Tume, kwa kupitia kituo kimoja na kurugenzi tatu kama ifuatavyo: Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia (CDTT), Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP), Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa (DKM) na Kurugenzi ya Huduma za Jamii (DCS)

Kwa upande wa Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia, Dk.Athman Mgumia alisema Kituo kinajishughulisha na masuala ya uhawilishaji wa teknolojia inayoibuka,maarifa ya ufundi kwa wazawa,utunzaji na usimamizi wa mazingira; miliki ya ubunifu,na tutoaji wa tuzo za sayansi na teknolojia.

Wakati Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP) Dk Bugwesa Katale alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya kuratibu na kuhamasisha utafiti, kutoa vipaumbele vya utafiti na kushauri uwekezaji wa fedha za utafiti. 

Pia alisema huongoza Mfuko wa Taifa wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) kupitia kamati za ufundi za utafiti na Maendeleo katika kuandaa ajenda za utafiti.

Alifafanua kuwa COSTECH ina Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa chini ya kaimu Mkurugenzi Dkt. Philbert Luhunga ambaye yeye alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya Ukusanyaji, Uhifadhi, na Usambazaji wa taarifa za Sayansi, Teknolojiana na Ubunifu.

 Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Jamii Anna Ngoo alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya Usimamizi wa Fedha,ukijumuisha, masuala ya Utumishi na Wafanyakazi, Utawala, Ruzuku ya Serikali na Ripoti za Wakaguzi.

Mkurugenzi Mkuu Dkt. Nungu alihitimisha kwa kuwashukuru Wajumbe wapya wa Bodi na kuwakaribisha COSTECH pamoja na kuwashukuru watoa mada wote kutoka katika

Kurugenzi za Tume.

EDITED
Picha ya pamoja ya Wajumbe wapya wa Bodi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia mara baada ya kumaliza Mafunzo kuhusu COSTECH

Learn More

UZINDUZI WA BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI (2020 - 2023)

Tume  ya  Taifa  ya  Sayansi  na  Teknolojia  siku  ya  Ijumaa  tarehe  17  Julai imezindua Baraza  jipya  la  wafanyakazi litakalodumu  kwa  kipindi  cha  miaka mitatu(2020 mpaka 2023)katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano ulipo Makao Makuu, Kinondoni Dar es salaam.

Kwa maelezo zaidi pakua hapa.

Learn More

TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa katika kuendeleza utamaduni wa kuadhimisha Siku ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu imeandaa Majadiliano maalum wa Kisayansi Siku Jumatatu ya tarehe 06 Julai, 2020, yenye kaulimbiu ya “Utafiti na Ubunifu ni Msingi wa Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.

Kwa maelezo zaidi, Soma zaidi hapa.

Learn More

Wadau wa Viwanda na Vyuo Vikuu Nchini wakutana Kujadili Mahusiano Yatakayoleta Tija katika Mageuzi ya Uchumi wa Viwanda Nchini

Tume  ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imeendesha Mdahalo kati ya  wadau wa Viwanda na Vyuo Vikuu ili kujadili kwa pamoja changamoto  zinazojitokeza katika eneo la mahusiano ili kuboresha mitaala ya elimu  na kujadili njia za kutatua changamoto na kuongeza kuongeza tija na  ufanisi pamoja na kasi ya uzalishaji wa ukuaji wa sekta ya viwanda  nchini.

Mdahalo  huo ulifunguliwa na Prof. Maulid Mwatawala Mwakilishi wa Makamu wa  Chuo cha Kilimo SUA, kwa kuwakaribisha wadau wote na amewataka  kuhakikisha wanaweka mikakati bora ya mahusiano ya pamoja ili kuendana  na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi kwa kuangalia  urasmishaji na  uhawilishaji wa Teknolojia kwa mandeleo ya viwanda nchini. Vilevile  kuangalia teknolojia zinazoakisi mazingira halisia ya nchi katika  kuongeza ushindani wa soko la ajira na umahiri wa wanafunzi/wahitimu  kukidhi mahitaji ya ukuaji wa sekta ya viwanda nchini. 


Wadau  mbalimbali waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa mdahalo huo na  kuwasilisha mada mbalimbali na kujadili changamoto kwa pamoja ni  kutoka  Vyuo Vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu Cha Kilimo SUA, kupitia (DPRTC)  ambayo ni Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhawawilishaji wa  Teknolojia na Ushauri wa Kitaalamu kupitia Kitengo cha “SUA Innovation  Hub” na Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Joseph- SJUIT kupitia idara ya ITAF,  Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT) na wadau wa Kongano (Cluster)  ya Mkoa wa Morogoro wanaofahamika kwa jina “Morogoro Food Processors  Clusters Initiative”


Aidha,  wawakilishi kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI)  inayosimamia  Sera na Ushawishi wa viwanda anaeleza ni muhimu kufanya tathimini ya  mahitaji “Training Need Assessment” ili kusaidia walimu na wanafunzi  kuendana na mazingira halisi. Kuahidi kuendelea kushirikiana na COSTECH  kama mshauri kwa kuwa kazi yao inategemea utafiti (Evidence based)  kuendesha shughuli zao.  Pia  Taasisi ya  wafanyabiashara wenye Viwanda, Biashara na Wakulima (TCCIA)  amesema  wanaendeleza mahusiano na Vyuo vikuu na viwanda kwa lengo la  kuwaunganisha ili  kuwapatia mafunzo kwa vitendo au uhalisia kwa kusudi la kukuza kada zao na uzoefu  wa ujasiriamali katika soko la ushindani la ndani na nje ya nchi. 


Akifunga  Mdahalo huu Dkt. Athumani Mgumia, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha  Uhawishaji wa Teknolojia (CDTT) ambae pia ni muwakilishi wa Mkurugenzi  Mkuu wa COSTECH amewashukuru wadau kwa kujitokeza na kujadili kwa pamoja  changamoto mbalimbali zinazojitokeza na amekaribisha mawazo yanayolenga  kufanya maboresho na kutoa mchango chanya kwa maendeleo endelevu ya  viwanda nchini.

Mdahalo  huu umeandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa  kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Taasisi.

Picha  ya Pamoja ya Washiriki wa Mdahalo wa Ubunifu na uboreshaji wa mahusiano  kati ya Vyuo vikuu na wadau wa Viwanda nchini. Siku ya Jumatano 17,  Juni 2020. Chuo Kikuu kilimo SUA, Mkoa wa Morogoro.


IMEANDALIWA NA;

AFISA UHUSIANO

TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH)

Learn More

Wadau wa Elimu Watakiwa Kutumia Bunifu Mbalimbali ili Kutatua Changamoto Zinazoikabili Sekta ya Elimu Nchini

Tume  ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imewakutanisha wabunifu  mbali mbali wa zana za kufundishia masomo ya sayansi na wadau wa Elimu  nchini. Kongamano hili lilofanyika katika ofisi za Taasisi ya Elimu  nchini (TAE) lilikuwa na lengo la kutatua changamoto mbali mbali ili  kuwezesha utumiaji wa bunifu zilizo buniwa kwa lengo la kurahisisha  ufundishaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari hapa nchini.

Akizindua  Kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Dkt.  Philbert Luhunga alielezea umuhimu wa matumizi ya bunifu hasa kwenye  sekta ya elimu. Dkt Luhunga aliwakaribisha washiriki na kuwasisitiza  kutatua changamoto zinazo sababisha kutokutumika kwa bunifu mbalimbali  zilizo buniwa na wabunifu wa hapa nchini. "Ubunifu wowote unakuwa na  tija unapotumika kutatua changamoto katika jamii, hivyo angalieni namna  bora ya kutumia bunifu hizi zenye lengo la kutatua changamoto kwenye  sekta ya Elimu" alishauri Dkt. Luhunga.

Kongamano  hilo lilihudhuriwa na wadau mbali mbali kutoka sekta ya Elimu wakiwamo  wawakilishi kutoka Taasisi ya HAKIELIMU, SHULE DIRECT, Shirika la umoja  wa mataifa linalojihusisha na maswala ya Sayansi (UNESCO)-Tanzania, Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam, na Mamlaka ya Elimu Tanzania.

Katika  Kongamano hilo bunifu mbali mbali za kufundishia masomo ya sayansi  ziliwasilishwa na kujadiliwa, baadhi ya bunifu hizo ni pamoja na ubunifu  wa SmartDarasa. Ubunifu huu unatumia njia za kieletroniniki na unaweza  kutumika kumfundisha mwanafunzi masomo ya sayansi kwa urahisi zaidi na  mwanafunzi kuelewa anachofundishwa kwa urahisi na wepesi zaidi. Ubunifu  mwingine uliowasilishwa unaitwa Jenga-Hub. Huu unajikita kuelimisha  watoto wenye umri wa kati ya miaka 7 mpaka 12  ili wawe na mawazo ya  kibunifu kwa lengo la kuwafanya kuwa wabunifu wa bunifu zenye tija hapo  baadae. 


Bunifu  nyingine zilizo wasilishwa ni pamoja na kifaa cha kieletroniki  kinachomwezesha mwanafunzi kujifunza kwa vitendo mzunguko wa kupatwa kwa  jua na mwezi kinachoitwa solar system electronics, ubunifu wa kutambua  uwezo wa kosa na kujifunza kwa kutumia kifaa cha kutoa sauti maalumu na  kifaa cha kufundishia mitaala ya elimu ya anga (Jua, Mwezi, Sayari na  Vimondo)

Bunifu zote hizo zilifadhiriwa na COSTECH kupitia mradi wa kukuza ubunifu (HDIF).

Akihitimisha  Kongamano hilo mwakilishi wa kamishna wa wizara ya Elimu alitoa  shukrani kwa COSTECH kwa kudhamini kongamano hilo na pia aliwasihi  wabunifu waendelee kushirikiana na wadau ili kuboresha eneo la  teknolojia na maudhui yanayoakisi elimu kwa vitendo nchini.


Washiriki    wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali  wa elimu na wabunifu   wa  zana za kufundishia masomo ya sayansi wakiwa  katika picha ya  pamoja   11/6/2020, Kinondoni, Dar es salaam.

Imetolewa na Afisa Uhusiano, 

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)

Learn More

BID call for proposals: Sub-Saharan Africa 2020

GBIF invites the submission of concept notes for project funding from sub-Saharan Africa through Biodiversity Information for Development (BID), a programme funded by the Directorate-General for International Partnerships of the European Union. 

For more Information please cllick here

DEADLINE: 27 AUGUST 2020

Learn More

CALL: COVID-19 AFRICA RAPID GRANT FUND

Call for Applicants - Researchers; Science and Health Journalists and Communicators; and Science AdvisersThe fight against the COVID-19 pandemic in Africa requires coordinated, responsive research as well as effective, evidence-based communication and science engagement.

Closing date is: 17 June 2020

Fore more information about the call please click here

For more information about framework application guidelines, please click here


Learn More

FURSA KWA WABUNIFU WA KITANZANIA

Mradi wa Kukuza Ubunifu Kusini mwa Africa (Southern Africa Innovation Support Program - SAIS 2) umetangaza fursa kwa wabunifu wa Kitanzania kutuma maombi ya kutangaza ubunifu wao.
Wabunifu wawili (2) watakaofuzu watawezeshwa kuhudhuria mafunzo ya ubunifu (bootcamp) jijini Helsinki, nchini Finland mwezi Novemba 2020.

Kama wewe ni mbunifu, au unamfahamu mbunifu aliyeko katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Arusha, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam, tafadhali mjulishe atembelee tangazo hilo kupitia: https://www.saisprogramme.org/connectedhubs/boostup

Fomu ya maombi inapatikana katika: https://drive.google.com/open?id=1nryrLZwK-Pay3YFGNAlYFG-iglbgYQ5-iWkdklxAkq4

kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:

https://www.saisprogramme.org

Learn More

Statement on Coronavirus Disease 2019 (COVID - 19)

Following the  unprecedented global outbreak of Coronavirus desease (COVID- 19), The Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) wishes to inform and advise its research stakeholders as follows: 

To read more informaiton please click here

Learn More

Extension of Application for ICGEB-DIC-MOST International Fellowship Program

Kindly note that due to the emergency situation and the difficulty in obtaining signatures/certificates and contacting prospective supervisors, the deadline for all Arturo Falaschi ICGEB Fellowship applications (long and short-term, SMART and also those relevant to the ICGEB-DIC-MOST International Fellowship Program) has been extended to 15 April 2020 (originally 31 March).


Barbara Argenti
Head, CRP & Fellowship Unit


For more information please click here.

Learn More

Kusitisha Kwa Muda Huduma Za Kumbi Za Mikutano

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Inapenda  kuwatangazia wateja na wadau wake wote kuwa imesitisha kwa muda kutoa  huduma za kukodisha kumbi zake zote kuanzia tarehe 23 Machi, 2020 hadi  itakapotangazwa hapo baadaye. Hii ni kutokana na Mlipuko wa virusi vya  Korona.
Anna G. Ngoo

Kny: MKURUGENZI MKUU

Learn More

Opportunity for Master in Bioethics Scholarships

The School of Bioethnics of Universidad Anahuac Mexico, responding to the need to prepare experts in the field of Global Bioethics. For more information please click here.

Learn More

2020 Research4Life Online Course

Research4Life is announcing online course for this year 2020. The deadline for applications is 7 April. Successful participants will be informed by 9 April 2020. For more informatiion, please click:  here

Learn More

Innovation Week 2020 - Dar Edition

Innovation Week 2020 is a series of events in Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya and Zanzibar curated by the Human Development Innovation Fund (HDIF) and COSTECH with support from UKAid and other partners and sponsors. The purpose of Innovation Week is to inspire current and future leaders in the country to take risks on new ideas, collaborate across sectors and transform Tanzania through the impact of innovation.

Fore More information Please click  here

The Opening ceremony will be officiated by Hon. Prof. Joyce Ndalichako, Minister of Education, Science and Technology and will take place at 9am on Monday the 9th of March at the Kisenga Hall LAPF Conference Centre. To view Full Schedule for the Opening ceremony and RSVP, please click here

Learn More

MAKISATU 2020

Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU 2020)

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na wadau wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wanapenda kuukaribisha Umma katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU 2020) yatakayofanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 20 Machi 2020.

Kwa maelezo zaidi soma bango hili.

Learn More

Watafiti nchini Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu za Kufanya Utafiti ili Zilete Tija kwa Taifa

Watafiti nchini wameshauriwa kuwasilisha andiko lolote la utafiti kwanza kwa wadau wa utafiti kabla ya kuomba kibali Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH ) ili wadau hao waweze kutoa ushauri wao kuhusu utafiti unaofanywa kwenye sekta yao na hivyo kufanya tafiti kuwa na tija zaidi kwa taifa.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu na taasisi za Utafiti na maendeleo nchini kujadili kuhusu maadili, Taratibu,Sheria na kanuni za kufanya utafiti nchini iliyoandaliwa na COSTECH kwenye ukumbi wa Taasisi ya elimu ya kujiendeleza kwenye Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Amesema ili tafiti ziweze kuleta tija zaidi na kuondoa changamoto za kurudia kufanya utafiti kuna kila sababu ya Watafiti kuwasilisha kwanza mawazo yao kwenye wizara au sekta husika kabla ya kupeleka maombi ya kufanya utafiti wowote kwenye Tume hiyo kwaajili ya kupitiwa na kupata kibali.

Dkt. Nungu amesema kumekuwa na lawama nyingi kwa baadhi ya watafiti kwamba vibali vya kufanya utafiti vinacheleweshwa na COSTECH kitu ambacho amesema inatokana na wao kuwasiliana na taasisi husika ama wadau wa utafiti kabla ya kupeleka kwenye kamati maalumu ya kitaifa kupitia na kuwapa ruksa ya kutoa kibali husika cha utafiti.

’’Mathalani unafanya utafiti kwenye Elimu tunategemea Utafiti wako utakuja kubadilisha ua kuboresha sera hivyo ni muhimu Wizara ya Elimu iweze kujua kinachofanyika ili nao waweze kutoa neno maana inawezekana ukafanya utafiti ambao majibu yao wanayo tayari’’ Alisema Dkt. Nungu.

Mkurugenzi huyo Mkuu wa COSTECH ameongeza kuwa eneo lingine ambalo wadau hao watajadiliana na kutoa mapendekezo ya pamoja ni namna ambavyo Mtafiti wa ndani anavyotakiwa kushiriki kwenye utafiti wa watu kutoka nje ya nchi hasa baada ya kugundua kuwa watafiti wa ndani huandikwa tu kwenye makaratasi kukithi vigezo vya kufanya utafiti lakini hawashiriki na hawafahamu lolote kuhusiana na hatua na utafiti unavyofanyika.

‘’ Taratibu za mtu kufanya utafiti kutoka nje ya nchi zinamtaka mtafiti huyo kuwa na mtafiti kutoka Tanzania lakini cha ajabu mtafiti wa ndani unapomuuliza kuhusu utafiti unavyoendelea na hatua zilizofikiwa hana majibu anakuambia anajua mtafiti wa nje kitu ambacho sio sawa katika taratibu za vibali vya kufanya tafiti za aina hizo’’ Alifafanua Dkt. Nungu.

Dkt. Nungu amesema haya na mambo mengine mengi ndiyo yaliyotufanya tukusanyike hapa kama wadau ili tuweze kufahamishana na kupeana ushauri wa namna ya kuboresha namna ya utendaj kazi kwenye eneo la utafiti ili ziweze kuleta tija nchini.

Kwa upande wake makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka ambaye ni mshirki wa warsha hiyo amesema utafiti unasaidia kutatua changamoto za nchi lakini pia lazima uzingatie vigezo na maadili ya kufanya taifi ili ulete tija kwa taifa.

Amesema ili Utafiti uingie na kutambuliwa na Taifa lazima upitie COSTECH ambao ndio waratibu wa tafiti zote ili kuweza kufikia malengo na serikali iweze kuutumia kwa manufaa ya jamii na Taifa badala ya watafiti kuishia kwenye taasisi zao kabla ya kushirikisha wadau.

Amesema kukutana kwao kwenye warsha hiyo kutasaidia sana wakuu wa taasisi kuweza kuwasaidia watafiti wake kutimiza vigenzo na masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za tafiti ili kuwa na Utafiti bora lakini pia kuwahisha kupata kibali kutoka COSTECH.
Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kiku cha Sokoine wakati wa Washa ya wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu na Taasisi za Utafiti wa Maendeleo.Learn More

ICGEB is Announcing for Postdoctoral Fellowships

International Centre for Genetic Engineering and Biotechnology ( ICGEB) is announcing the Arturo Falaschi Fellowships Programme: Postgradoctoral Fellowships.

The closing date for applicaiton is: 31st March and 30 September 2020. For more informaiton, please click here

Learn More

Shortlisted Applicants in Second Round of Business Plan Innovation Challenge

Tanzania Digital Innovation Youth Empowerment Programme (TADIYE) is an innovation and entrepreneurship ecosystem development initiative, designed to inspire and promote technology-based young start up entrepreneurs in Tanzania. The project is funded by the Royal Danish Embassy in Tanzania and implemented through Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) in collaboration with two other key partners; Magilatech Company Limited and Institute for Management and Entrepreneurship Development (IMED)

For more information please clicks the link below In:

Swahili

English

Learn More

DISCOVER INCUBATORS

The Commission for Science and Technology has information about incubators in Tanzania.


Learn More

OPEN CALLS FOR PROPOSAL

The Commission for Science and Technology Calls for Proposal module


Learn More

RESEARCH PROJECTS & PUBLICATIONS

The Commission for Science and Technology Research projects and module


Learn More

RESEARCH CLEARENCE MODULE

The Commission for Science and Technology Research clearance module


Learn More

COSTECH ORGANOGRAM

The Commission for Science and Technology Organogram includes the four directorates.


Learn More