Nomination for Women in Technology Awards
Here is your chance to nominate outstanding women in technology and ICT who are breaking boundaries in a Men's led area.
Working in Innovations, Inventors or enablers in innovation who have been able to uplift other women. The awards will be presented during the women
in Technology festival organized by @BuniDicaz and @ COSTECH
Deadline is 10th April, 2021
For more information please click here
HEET Documents
Please find below documents for HIgher Education for Economic Transformation Project (HEET).
1. Resettlement Policy Framework (RPF)
2. Environmental and Social Management Framework (ESMF)
CALL FOR APPLICATIONS FOR THE WORLD TRADE ORGANISATION CHAIRS PROGRAMME
The Ministry of Education, Science and Technology (MoEST) received a diplomatic notification from the Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation informing that the World Trade Organisation (WTO) launched the third phase of its Chairs Programme. The aim of the programme is to support and promote trade-related academic activities by enhancing knowledge and understanding of the multilateral trading system among academics and policy makers in beneficiary countries.
WTO invites Universities and Research Institutions in Developing countries to apply financial, scientific and technical support for research, curriculum development and outreach activities.
Institutions are required to submit an online expression of interest form and an online application form by 15th January, 2021. The application deadline was 15 January 2021, it has been extended to 15 February 2021. The expression of interest form can be accessed via this link. And the online application form can be accessed via this link. For more information you can contact: wtochairs@wto.org.
COSTECH Yatoa Mafunzo Kwa Waandishi wa Habari Jinsi ya Kuandika Habari za Utafiti wa Sayansi
Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH nimetoa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari na watafiti jijini Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo namna ya kuandika habari za kisayansi ili ziweze kuwafikia walaji kwa njia rahisi kwa kutumia wanahabari.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo yaliyofanyika Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa kutoka COSTECH Dkt Philibert Luhunga amesema lengo ni kuona Teknolojia ya Sayansi inayobuniwa na Watafiti inawafikia wananchi au walaji kwa lugha rahisi.
Alisema, Lengo la kuwakutanisha ni kutengeneza mahusiano mazuri baina ya waandishi na Watafiti ili kuwezesha tafiti mbalimbali zinazofanywa na hawa watafiti ziwafikie wananchi kiurahisi kwa sababu tafiti hizo zinakuwa katika Lugha ya Sayansi, lakini tafiti hizo zikipelekwa kwa wananchi kwa kutumia wanahabari ni rahisi kueleweka na walaji wa tafiti hizo.
Aidha Dkt. Luhunga amewataka waandishi wa habari kuandika mara kwa mara habari zinazohusu Sayansi hasa tafiti zinazofanywa na wataalamu wetu ili wananchi wanufanike na tafiti zinazofanywa na wataalamu wetu.
Alisisitiza hasa katika kipindi hiki nchi imejikita katika uchumi wa viwanda Teknolojia za ndani ni muhimu sana katika maendeleo ya Taifa ili kama nchi tufikie azma ya kuwa nchi ya Viwanda.
Vilevile amesema kuwa mpaka sasa wameshafanya semina kama hizo katika Mikoa ya Dar es saalam, Tanga, Mtwara na Unguja na katika maeneo hayo kumeonekana matokeo chanya kwa waandishi kuwa na mwamko mkubwa wa kuripoti na kuandika habari za utafiti mbalimbali.
Alisema “Kote ambako tumefanya semina kama hizi kumeonyesha mwamko mkubwa sana wa kuripoti taarifa za sayansi na kitafiti zilizosaidia kuokoa maisha ya watu, hasa tafiti za hali ya hewa kwa kanda ya mashariki”.
Aidha amewashauri wananchi kuendelea kufuatilia habari za utafiti wa kisayansi katika nyanja mbalimbali na wasisite kuwasiliana na Mamlaka husika wanapoona mabadiliko ya kisayansi katika maeneo yao.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Makutupora Dkt. Cornel Masawe amesema waandishi wa habari ni watu muhimu katika kufanikisha usambaaji wa tafiti za kisayansi ili kuwafikia walengwa wa tafiti hizo.
Amesema kwa upande wa TARI wana takribani vituo kumi na saba (17) nchi nzima ambavyo vinafanya utafiti wa mbegu mbalimbali za mazao na wamekuwa wakizalisha teknolojia tofauti tofauti za mbegu za kilimo zinazoweza kuwanufaisha wakulima hapa nchini.
Alimalizia kwa kusema kuwa hapo mwanzo walikuwa wakitumia siku ya nane nane (Siku kuu ya wakulima nchini) ili kutangaza tafiti zao tukio lililokuwa likifanyika mara moja kwa mwaka lakini kwa sasa wamefungua ofisi katika kanda zote hapa nchini ambapo anaamini baada ya mafunzo haya waandishi wa habari wataminiminika kwenye ofisi zao kutaka kujua tafiti zinazofanywa.
Mafunzo haya yalifanyika katika ukumbi wa airport ambayo yameshirikisha washiriki arobaini (40) kati yao kumi na sita (16) walikuwa watafiti kutoka taasisi za utafiti na washiriki ishirini na nne (24) walikuwa ni waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Menejiment ya Maarifa akifungua mafunzo ya watafiti na
Waandishi wa habari.
Mwezeshaji wa mafunzo ya watafiti na waandishi wa habari Dr. Dietrick Kaijanangoma
akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akitoa mafunzo hayo.
MASHINDANO YA KITAIFA YA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU (MAKISATU 2021)
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawaalika Watanzania wenye Ubunifu, Ugunduzi na Maarifa Asilia kushiriki katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kwa mwaka 2021.
Kwa maelezo zaidi tafadhali bobya hapa
Professional Librarians Need to Rebrand themselves for Rapidly Increase Digital Collection of Information’s
The Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) conducted a training for professional librarians to explore the advantage of rapidly increasing collection of digital information, web based environment and associated sophisticated tool to serve the new information-based society.
The training oriented professional librarians to change traditional gatekeeping of printed knowledge products to advance level of managing electronic knowledge products taking advantage of progression in Science and Technology.
Either the training had equipped librarians with the knowledge on using information system in managing the library activities and sharing the resources among Research and Development institutions (R&Ds) and Higher Learning Institutions (HLIs). Also the training equipped them with the knowledge on how to use information systems in disseminating information to the potential users and increase access of information to the public.
Due to that a total of 13 participant’s improved knowledge and skills on e-Library technologies, sharing experience among professional Librarians from R&Ds and HLIs on e-library management and created R&Ds and HLIs WhatsApp group for Librarians for easy communication and problem solving on the use of e-Library.
During this training about eight (8) libraries from R&Ds and HLIs such as National Development Corporation (NDC), Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC), Tanzania Agriculture Research Institute (TARI) - Naliendele, National Construction Council (NCC), Tropical Pesticides Research Institute (TPRI), National Environment Management Council (NEMC), Tanzania Bureau Standards (TBS) and Tanzania Meteorological Authority (TMA) were attended and connected to COSTECH e- library.
The training was held at Bagamoyo from 10th from 14 of November, 2020.
Launch Invitation: O.R Tambo Africah Research Chairs Initiative
You are warmly invited to the virtual O.R. Tambo Africa Research Chairs Initiative Launch.
You are warmly invited to the virtual O.R. Tambo Africa Research Chairs Initiative Launch as follows:
Date: 27 October 2020
Time: 14h30 – 16h30 (CAT)
Venue: Online connection details will be communicated with registered attendees
Since 2017, the National Research Foundation of South Africa (NRF), South Africa’s Department of Science and Innovation (DSI), the International Development Research Centre (IDRC) Canada, the Oliver & Adelaide Tambo Foundation, and participating councils of the Science Granting Councils Initiative in Sub-Saharan Africa (SGCI) have been partnering to implement the O.R. Tambo Africa Research Chairs Initiative (ORTARChI).
This virtual event will launch the first ten (10) host institutions and research chairholders across seven (7) countries in sub-Saharan Africa, in recognition of excellence, individual leadership and talent, and the commitment of universities to supporting high-quality research. This will be followed by a high-level panel discussion on Investing in Research and Innovation Excellence in Africa. This launch marks the 103rd birthday of Oliver Tambo.
For more information and to register for the event, please click here or visit https://www.nrf.ac.za/or_tambo_africa_research_chairs_initiative_launch/
Best regards
ORTARChI Team
|
|
https://www.nrf.ac.za/email-legal-notice.php
MPANGO WA O.R. TAMBO KUHUSU VIGODA VYA UTAFITI AFRIKA: KUTANA NA TIMU INAYOLENGA KUFANYA MABADILIKO YA MAZINGIRA YA UTAFITI BARANI AFRIKA.
Pretoria Afrika ya Kusini: Mpango wa Vigoda vya Utafiti Afrika (Africa Research Chairs Initiative (ORTARChI), unayo furaha kukutaarifu kuwa imechagua taasisi kumi na watafiti wenyeviti ambao ni waanzilishi wa awamu ya kwanza ya programu hiyo. Mpango huu ulioanzishwa na Mfuko wa Utafiti wa Afrika ya Kusini (National Research Foundation - NRF) Idara ya Sayansi na Ubunifu (Department of Science and Innovation - DSI) kwa ushirikiano na Mfuko wa Oliver & Adelaide Tambo (OATF), Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo ya Utafiti, Canada (Canada’s International Development Research Centre - IRDC) na Mabaraza Saba ya Maendeleo ya Sayansi, yaliyoko kusini mwa jangwa la Sahara (seven councils of the Science Granting Councils Initiative in Sub-Saharan Africa - SGCI).
Kwa maelezo zaidi bofya hapa
COSTECH Yashiriki Uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Utafiti Kuhusu Mazingira
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeshiriki warsha ya kuhuisha Ajenda ya Taifa ya Utafiti wa Mazingira (NERA), inayosimamiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kupitia Kamati ya Ushauri wa Utafiti kuhusu Mazingira (ERAC).
Warsha hiyo imefanyika katika Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro kuanzia tarehe 7 -8 Oktoba, 2020 ambapo washiriki wa Warsha hiyo ni wajumbe wa kamati kutoka katika Vyuo Vikuu, Sekta binafsi, Tawala za Mikoa na Taasisi mbalimbali zinazohusika na mazingira kutoka Tanzania Bara na Visiwani ambapo COSTECH ni mjumbe wa kamati hiyo.
Lengo la warsha hiyo ni kuzindua Kamati ya Ushauri wa Tafiti zinazohusu Mazingira pamoja na kuwapitisha wajumbe hao katika Ajenda ya Taifa ya Utafiti wa Mazingira 2017 – 2022 ili waweze kuifanyia maboresho.
Katika warsha hiyo, COSTECH iliwakilishwa na Bwana Merchades Rutechura ambaye aliwasilisha mada kuhusu “Nafasi ya Tume katika kuratibu na kuhamasisha tafiti zinazohusu Mazingira.”
Aidha, katika mawasilisho hayo, COSTECH iliainisha miradi ya utafiti na ubunifu iliyowahi kufadhiliwa kwa kipindi kilichoanzia mwaka 2015 – 2020; mafanikio yaliyopatikana; changamoto zinazoikumba Tume katika kuratibu na kuhamasisha tafiti zinazohusu Mazingira pamoja na njia inazotumia kutatua changamoto hizo.
Vilevile warsha hiyo iliambatana na uchaguzi wa Mwenyekiti wa ERAC ambapo Bw. Thomas Bwana kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Idara ya Mazingira alichaguliwa kuongoza Kamati kwa kipindi cha miaka mitatu (3).
Warsha ilifunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Mhandisi Samuel Gwamaka Mafwenga.
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Utafiti kuhusu Mazingira kutoka Vyuo Vikuu, Sekta binafsi, Tawala za Mikoa na Taasisi mbalimbali zinazohusika na mazingira kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Watafiti Waahidi Kukamilisha Miongozo ya Kamati za Kusimamia Maadili ya Tafiti Katika Taasisi Zao
Watafiti kutoka katika Taasisi za tafiti nchini ambazo ni Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), Taasisi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) waahidi kukamilisha miongozo ya kamati za kusimamia maadili ya utafiti katika taasisi zao.
Watafiti hao wameyasema hayo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu alipokuwa akifungua kikao Kazi cha kuandaa miongozo ya Kamati za kusimamia maadili ya Utafiti. Kikao hicho kinachofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Uongozi wa Elimu (ADEM) Bagamoyo na kimeandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) chini ya Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP).
Akifungua kikao kazi hicho Dkt. A. Nungu alisema anatamani ifikapo mwezi wa Novemba mwaka huu wa 2020 amualike Waziri kwaajili ya kuzindua miongozo yetu kutoka katika taasisi zetu za utafiti ambazo ni TALIRI, TARI, TAFORI na TAFIRI.
Dkt. Nungu alisema, COSTECH inajitahidi kujenga uwezo katika taasisi za tafiti ili ziweze kusaidia kufanya kazi kwa urahisi zaidi.
Aidha kikao kazi hiki kina jumla ya wawakilishi kumi na sita (16) kutoka katika taasisi nne ambazo kila taasisi ilileta wawakilishi wanne (4) ili kushiriki kwa pamoja katika kikao kazi hicho cha kutengeneza miongozo ya kamati za kusimamia maadili ya utafiti.
Lengo la kikao kazi hiki ni kuwajengea uwezo Taasisi zinazojishughulisha na tafiti nchini ili ziweze kufuata taratibu na kuzingatia miongozo ya kamati za maadili ya utafiti na hatimaye kutumia matokeo ya tafiti kujibu changamoto zinazojitokeza katika jamii yetu.
Washiriki mbalimbali walieleza jinsi wanavyotekeleza majukumu yao kisheria na kuonesha uhitaji wa kupata miongozo (Standard Operating Procedure) zitakazowaongoza ili kufanikisha shughuli za utafiti na kutengeneza kamati za maadili ya kusimamia utafiti katika Taasisi zao.
Dkt. Nungu aliwapongeza kwa Kazi nzuri inayoendelea kufanywa na wadau huku akisisitiza jukumu la kimsingi la utoaji wa vibali na kuwatakia kikao kazi chema chenye mafanikio.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Amos Nungu wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha kuandaa Miongozo ya kamati za kuasimamia maadili ya utafiti yaliofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Maendeleo Uongozi wa Elimu (ADEM) – Bagamoyo.
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Kufanya Maboresho ya Mfumo wa Kusimamia Tafiti na Bunifu
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu amesisitiza ushiriki wa pamoja kwa wataalamu wa ndani na kusema kwamba hiyo itasaidia kuboresha mfumo.
Hayo aliyasema wakati akifungua Kikao cha Kikosikazi cha Maboresho ya Mfumo wa kielektroniki wa Utafiti na Ubunifu jana katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo iliyoko Mikocheni (MARI), jijini Dar es Salaam.
Dkt. Nungu alisema kutokana na hilo hawana budi kujitahidi kwenda na wakati ili wanapomaliza maboresho ya mfumo wao kusitokee matatizo ya kimfumo hapo baadaye.
Akielezea katika kikao hicho Meneja wa Kitengo cha TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Ndugu Emmanuel Nnko amesema tupo katika jitihada za maboresho ya mfumo wa ndani ambao utasaidia kuiwezesha Tume kusimamia na kudhibiti utaratibu mzima wa utafiti na ubunifu katika maeneo mawili, kwanza ni kutoa vibali vya miradi ya utafiti na pili kutoa ufadhili kwa wabunifu.
Vilevile amesema kwasasa wataalamu wapo katika sehemu ya awali ya ukusanyaji wa mahitaji kutoka kwa watumiaji ili kuhakikisha mahitaji yote yanaingizwa kwenye mfumo na sehemu ya pili ni maendeleo ya mfumo ya kufanikisha mahitaji hayo.
Katika Kikao hicho washiriki walioshiriki mpaka sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Wakurugenzi wa Idara mbalimbali ikiwemo Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia (CDTT), Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP) na Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa (DKM) pamoja na wadau kutoka taasisi nyingine kama TANESCO na NIDA ili kufanya maboresho ya Mfumo wa Tafiti na Ubunifu.
Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na wataalamu kutoka NIDA katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha kuboresha mfumo wa kusimamia Tafiti na bunifu
Call for Proposals: Grants for Regional Innovation Projects
The Southern Africa Innovation Support Programme (SAIS 2) Innovation fund is inviting project proposals for funding through the RE:innovation challenge competition. RE:innovation is a challenge inspired by recent events.
Deadline for application is: 27th September, 2020 at 23:59 CAT
For more infomation about the call please click here
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Yatoa Mafunzo Kuhusu COSTECH kwa Wajumbe Wapya wa Bodi
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetoa mafunzo kwa Wajumbe wapya wa Bodi kuhusu Tume (COSTECH).
Mafunzo hayo yalitolewa hivi karibuni katika ukumbi mdogo wa COSTECH, yalifunguliwa na Mkurugegenzi wa COSTECH Dkt. Amos Nungu.
Dkt. Nungu aliwakaribisha wajumbe wapya wa Bodi na baadaye kuwakaribisha wakuu wa idara ili kuweza kuwapitisha kwa ufupi wajumbe hao wapya ili waweze kuelewa majukumu ya Tume kwa ujumla.
Akielezea muhtasari wa COSTECH Kaimu Meneja Kitengo cha Huduma za Sheria Bw. Ernest Barulo alisema, Shughuli zaTume ya Taifaya Sayansi naTeknolojia zilianzishwa rasmimwaka 1972 chini yaBaraza la ufafiti (Tanzania National Scientific Research Council) kwa kifupiUTAFITI, lakini mwaka1988 lilibadilishwa kuwa Tumeya Taifa ya Sayansina Teknolojia kwa kifupi (COSTECH) kwamujibu wa sheria Na.7ya bunge ya mwaka 1986.
Bw. Barulo alisema majukumu Makuu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ni pamoja na kuishauri Serikali kuhusu mambo yote yanayohusu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na matumizi yake katika maendeleo Kiuchumi na Kijamii nchini.
Aidha sekretariati inasimamia utendaji wake wa kila siku wa Tume, kwa kupitia kituo kimoja na kurugenzi tatu kama ifuatavyo: Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia (CDTT), Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP), Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa (DKM) na Kurugenzi ya Huduma za Jamii (DCS)
Kwa upande wa Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia, Dk.Athman Mgumia alisema Kituo kinajishughulisha na masuala ya uhawilishaji wa teknolojia inayoibuka,maarifa ya ufundi kwa wazawa,utunzaji na usimamizi wa mazingira; miliki ya ubunifu,na tutoaji wa tuzo za sayansi na teknolojia.
Wakati Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP) Dk Bugwesa Katale alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya kuratibu na kuhamasisha utafiti, kutoa vipaumbele vya utafiti na kushauri uwekezaji wa fedha za utafiti.
Pia alisema huongoza Mfuko wa Taifa wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) kupitia kamati za ufundi za utafiti na Maendeleo katika kuandaa ajenda za utafiti.
Alifafanua kuwa COSTECH ina Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa chini ya kaimu Mkurugenzi Dkt. Philbert Luhunga ambaye yeye alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya Ukusanyaji, Uhifadhi, na Usambazaji wa taarifa za Sayansi, Teknolojiana na Ubunifu.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Jamii Anna Ngoo alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya Usimamizi wa Fedha,ukijumuisha, masuala ya Utumishi na Wafanyakazi, Utawala, Ruzuku ya Serikali na Ripoti za Wakaguzi.
Mkurugenzi Mkuu Dkt. Nungu alihitimisha kwa kuwashukuru Wajumbe wapya wa Bodi na kuwakaribisha COSTECH pamoja na kuwashukuru watoa mada wote kutoka katika
Kurugenzi za Tume.
Picha ya pamoja ya Wajumbe wapya wa Bodi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia mara baada ya kumaliza Mafunzo kuhusu COSTECH
UZINDUZI WA BARAZA JIPYA LA WAFANYAKAZI (2020 - 2023)
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia siku ya Ijumaa tarehe 17 Julai imezindua Baraza jipya la wafanyakazi litakalodumu kwa kipindi cha miaka mitatu(2020 mpaka 2023)katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano ulipo Makao Makuu, Kinondoni Dar es salaam.
Kwa maelezo zaidi pakua hapa.
TAARIFA KWA UMMA
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa katika kuendeleza utamaduni wa kuadhimisha Siku ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu imeandaa Majadiliano maalum wa Kisayansi Siku Jumatatu ya tarehe 06 Julai, 2020, yenye kaulimbiu ya “Utafiti na Ubunifu ni Msingi wa Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.
Kwa maelezo zaidi, Soma zaidi hapa.
Wadau wa Viwanda na Vyuo Vikuu Nchini wakutana Kujadili Mahusiano Yatakayoleta Tija katika Mageuzi ya Uchumi wa Viwanda Nchini
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imeendesha Mdahalo kati ya wadau wa Viwanda na Vyuo Vikuu ili kujadili kwa pamoja changamoto zinazojitokeza katika eneo la mahusiano ili kuboresha mitaala ya elimu na kujadili njia za kutatua changamoto na kuongeza kuongeza tija na ufanisi pamoja na kasi ya uzalishaji wa ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
Mdahalo huo ulifunguliwa na Prof. Maulid Mwatawala Mwakilishi wa Makamu wa Chuo cha Kilimo SUA, kwa kuwakaribisha wadau wote na amewataka kuhakikisha wanaweka mikakati bora ya mahusiano ya pamoja ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiuchumi kwa kuangalia urasmishaji na uhawilishaji wa Teknolojia kwa mandeleo ya viwanda nchini. Vilevile kuangalia teknolojia zinazoakisi mazingira halisia ya nchi katika kuongeza ushindani wa soko la ajira na umahiri wa wanafunzi/wahitimu kukidhi mahitaji ya ukuaji wa sekta ya viwanda nchini.
Wadau mbalimbali waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa mdahalo huo na kuwasilisha mada mbalimbali na kujadili changamoto kwa pamoja ni kutoka Vyuo Vikuu nchini kikiwepo Chuo Kikuu Cha Kilimo SUA, kupitia (DPRTC) ambayo ni Kurugenzi ya Uzamili, Utafiti, Uhawawilishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalamu kupitia Kitengo cha “SUA Innovation Hub” na Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Joseph- SJUIT kupitia idara ya ITAF, Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT) na wadau wa Kongano (Cluster) ya Mkoa wa Morogoro wanaofahamika kwa jina “Morogoro Food Processors Clusters Initiative”
Aidha, wawakilishi kutoka Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) inayosimamia Sera na Ushawishi wa viwanda anaeleza ni muhimu kufanya tathimini ya mahitaji “Training Need Assessment” ili kusaidia walimu na wanafunzi kuendana na mazingira halisi. Kuahidi kuendelea kushirikiana na COSTECH kama mshauri kwa kuwa kazi yao inategemea utafiti (Evidence based) kuendesha shughuli zao. Pia Taasisi ya wafanyabiashara wenye Viwanda, Biashara na Wakulima (TCCIA) amesema wanaendeleza mahusiano na Vyuo vikuu na viwanda kwa lengo la kuwaunganisha ili kuwapatia mafunzo kwa vitendo au uhalisia kwa kusudi la kukuza kada zao na uzoefu wa ujasiriamali katika soko la ushindani la ndani na nje ya nchi.
Akifunga Mdahalo huu Dkt. Athumani Mgumia, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uhawishaji wa Teknolojia (CDTT) ambae pia ni muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH amewashukuru wadau kwa kujitokeza na kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazojitokeza na amekaribisha mawazo yanayolenga kufanya maboresho na kutoa mchango chanya kwa maendeleo endelevu ya viwanda nchini.
Mdahalo huu umeandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya Taasisi.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mdahalo wa Ubunifu na uboreshaji wa mahusiano kati ya Vyuo vikuu na wadau wa Viwanda nchini. Siku ya Jumatano 17, Juni 2020. Chuo Kikuu kilimo SUA, Mkoa wa Morogoro.
IMEANDALIWA NA;
AFISA UHUSIANO
TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH)
Wadau wa Elimu Watakiwa Kutumia Bunifu Mbalimbali ili Kutatua Changamoto Zinazoikabili Sekta ya Elimu Nchini
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imewakutanisha wabunifu mbali mbali wa zana za kufundishia masomo ya sayansi na wadau wa Elimu nchini. Kongamano hili lilofanyika katika ofisi za Taasisi ya Elimu nchini (TAE) lilikuwa na lengo la kutatua changamoto mbali mbali ili kuwezesha utumiaji wa bunifu zilizo buniwa kwa lengo la kurahisisha ufundishaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari hapa nchini.
Akizindua Kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Dkt. Philbert Luhunga alielezea umuhimu wa matumizi ya bunifu hasa kwenye sekta ya elimu. Dkt Luhunga aliwakaribisha washiriki na kuwasisitiza kutatua changamoto zinazo sababisha kutokutumika kwa bunifu mbalimbali zilizo buniwa na wabunifu wa hapa nchini. "Ubunifu wowote unakuwa na tija unapotumika kutatua changamoto katika jamii, hivyo angalieni namna bora ya kutumia bunifu hizi zenye lengo la kutatua changamoto kwenye sekta ya Elimu" alishauri Dkt. Luhunga.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wadau mbali mbali kutoka sekta ya Elimu wakiwamo wawakilishi kutoka Taasisi ya HAKIELIMU, SHULE DIRECT, Shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na maswala ya Sayansi (UNESCO)-Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Katika Kongamano hilo bunifu mbali mbali za kufundishia masomo ya sayansi ziliwasilishwa na kujadiliwa, baadhi ya bunifu hizo ni pamoja na ubunifu wa SmartDarasa. Ubunifu huu unatumia njia za kieletroniniki na unaweza kutumika kumfundisha mwanafunzi masomo ya sayansi kwa urahisi zaidi na mwanafunzi kuelewa anachofundishwa kwa urahisi na wepesi zaidi. Ubunifu mwingine uliowasilishwa unaitwa Jenga-Hub. Huu unajikita kuelimisha watoto wenye umri wa kati ya miaka 7 mpaka 12 ili wawe na mawazo ya kibunifu kwa lengo la kuwafanya kuwa wabunifu wa bunifu zenye tija hapo baadae.
Bunifu nyingine zilizo wasilishwa ni pamoja na kifaa cha kieletroniki kinachomwezesha mwanafunzi kujifunza kwa vitendo mzunguko wa kupatwa kwa jua na mwezi kinachoitwa solar system electronics, ubunifu wa kutambua uwezo wa kosa na kujifunza kwa kutumia kifaa cha kutoa sauti maalumu na kifaa cha kufundishia mitaala ya elimu ya anga (Jua, Mwezi, Sayari na Vimondo)
Bunifu zote hizo zilifadhiriwa na COSTECH kupitia mradi wa kukuza ubunifu (HDIF).
Akihitimisha Kongamano hilo mwakilishi wa kamishna wa wizara ya Elimu alitoa shukrani kwa COSTECH kwa kudhamini kongamano hilo na pia aliwasihi wabunifu waendelee kushirikiana na wadau ili kuboresha eneo la teknolojia na maudhui yanayoakisi elimu kwa vitendo nchini.
Washiriki wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu na wabunifu wa zana za kufundishia masomo ya sayansi wakiwa katika picha ya pamoja 11/6/2020, Kinondoni, Dar es salaam.
Imetolewa na Afisa Uhusiano,
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)
BID call for proposals: Sub-Saharan Africa 2020
GBIF invites the submission of concept notes for project funding from sub-Saharan Africa through Biodiversity Information for Development (BID), a programme funded by the Directorate-General for International Partnerships of the European Union.
For more Information please cllick here
DEADLINE: 27 AUGUST 2020
CALL: COVID-19 AFRICA RAPID GRANT FUND
Call for Applicants - Researchers; Science and Health Journalists and Communicators; and Science Advisers
The fight against the COVID-19 pandemic in Africa requires coordinated, responsive research as well as effective, evidence-based communication and science engagement.
Closing date is: 17 June 2020
Fore more information about the call please click here
For more information about framework application guidelines, please click here
FURSA KWA WABUNIFU WA KITANZANIA
Mradi wa Kukuza Ubunifu Kusini mwa Africa (Southern Africa Innovation Support Program - SAIS 2) umetangaza fursa kwa wabunifu wa Kitanzania kutuma maombi ya kutangaza ubunifu wao.
Wabunifu wawili (2) watakaofuzu watawezeshwa kuhudhuria mafunzo ya ubunifu (bootcamp) jijini Helsinki, nchini Finland mwezi Novemba 2020.
Kama wewe ni mbunifu, au unamfahamu mbunifu aliyeko katika mikoa ya Iringa, Mbeya, Arusha, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam, tafadhali mjulishe atembelee tangazo hilo kupitia: https://www.saisprogramme.org/connectedhubs/boostup
Fomu ya maombi inapatikana katika: https://drive.google.com/open?id=1nryrLZwK-Pay3YFGNAlYFG-iglbgYQ5-iWkdklxAkq4
kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea:
Statement on Coronavirus Disease 2019 (COVID - 19)
Following the unprecedented global outbreak of Coronavirus desease (COVID- 19), The Tanzania Commission for Science and Technology (COSTECH) wishes to inform and advise its research stakeholders as follows:
To read more informaiton please click here
Extension of Application for ICGEB-DIC-MOST International Fellowship Program
Kindly note that due to the emergency situation and the difficulty in obtaining signatures/certificates and contacting prospective supervisors, the deadline for all Arturo Falaschi ICGEB Fellowship applications (long and short-term, SMART and also those relevant to the ICGEB-DIC-MOST International Fellowship Program) has been extended to 15 April 2020 (originally 31 March).
Barbara Argenti
Head, CRP & Fellowship Unit
For more information please click here.
Kusitisha Kwa Muda Huduma Za Kumbi Za Mikutano
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Inapenda kuwatangazia wateja na wadau wake wote kuwa imesitisha kwa muda kutoa huduma za kukodisha kumbi zake zote kuanzia tarehe 23 Machi, 2020 hadi itakapotangazwa hapo baadaye. Hii ni kutokana na Mlipuko wa virusi vya Korona.
Anna G. Ngoo
Kny: MKURUGENZI MKUU
Opportunity for Master in Bioethics Scholarships
The School of Bioethnics of Universidad Anahuac Mexico, responding to the need to prepare experts in the field of Global Bioethics. For more information please click here.
2020 Research4Life Online Course
Research4Life is announcing online course for this year 2020. The deadline for applications is 7 April. Successful participants will be informed by 9 April 2020. For more informatiion, please click: here
Innovation Week 2020 - Dar Edition
Innovation Week 2020 is a series of events in Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya and Zanzibar curated by the Human Development Innovation Fund (HDIF) and COSTECH with support from UKAid and other partners and sponsors. The purpose of Innovation Week is to inspire current and future leaders in the country to take risks on new ideas, collaborate across sectors and transform Tanzania through the impact of innovation.
Fore More information Please click here
The Opening ceremony will be officiated by Hon. Prof. Joyce Ndalichako, Minister of Education, Science and Technology and will take place at 9am on Monday the 9th of March at the Kisenga Hall LAPF Conference Centre. To view Full Schedule for the Opening ceremony and RSVP, please click here
MAKISATU 2020
Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU 2020)
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja na wadau wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wanapenda kuukaribisha Umma katika Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU 2020) yatakayofanyika Jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 20 Machi 2020.
Kwa maelezo zaidi soma bango hili.
Watafiti nchini Watakiwa Kufuata Sheria na Taratibu za Kufanya Utafiti ili Zilete Tija kwa Taifa
Watafiti nchini wameshauriwa kuwasilisha andiko lolote la utafiti kwanza kwa wadau wa utafiti kabla ya kuomba kibali Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH ) ili wadau hao waweze kutoa ushauri wao kuhusu utafiti unaofanywa kwenye sekta yao na hivyo kufanya tafiti kuwa na tija zaidi kwa taifa.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu na taasisi za Utafiti na maendeleo nchini kujadili kuhusu maadili, Taratibu,Sheria na kanuni za kufanya utafiti nchini iliyoandaliwa na COSTECH kwenye ukumbi wa Taasisi ya elimu ya kujiendeleza kwenye Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Amesema ili tafiti ziweze kuleta tija zaidi na kuondoa changamoto za kurudia kufanya utafiti kuna kila sababu ya Watafiti kuwasilisha kwanza mawazo yao kwenye wizara au sekta husika kabla ya kupeleka maombi ya kufanya utafiti wowote kwenye Tume hiyo kwaajili ya kupitiwa na kupata kibali.
Dkt. Nungu amesema kumekuwa na lawama nyingi kwa baadhi ya watafiti kwamba vibali vya kufanya utafiti vinacheleweshwa na COSTECH kitu ambacho amesema inatokana na wao kuwasiliana na taasisi husika ama wadau wa utafiti kabla ya kupeleka kwenye kamati maalumu ya kitaifa kupitia na kuwapa ruksa ya kutoa kibali husika cha utafiti.
’’Mathalani unafanya utafiti kwenye Elimu tunategemea Utafiti wako utakuja kubadilisha ua kuboresha sera hivyo ni muhimu Wizara ya Elimu iweze kujua kinachofanyika ili nao waweze kutoa neno maana inawezekana ukafanya utafiti ambao majibu yao wanayo tayari’’ Alisema Dkt. Nungu.
Mkurugenzi huyo Mkuu wa COSTECH ameongeza kuwa eneo lingine ambalo wadau hao watajadiliana na kutoa mapendekezo ya pamoja ni namna ambavyo Mtafiti wa ndani anavyotakiwa kushiriki kwenye utafiti wa watu kutoka nje ya nchi hasa baada ya kugundua kuwa watafiti wa ndani huandikwa tu kwenye makaratasi kukithi vigezo vya kufanya utafiti lakini hawashiriki na hawafahamu lolote kuhusiana na hatua na utafiti unavyofanyika.
‘’ Taratibu za mtu kufanya utafiti kutoka nje ya nchi zinamtaka mtafiti huyo kuwa na mtafiti kutoka Tanzania lakini cha ajabu mtafiti wa ndani unapomuuliza kuhusu utafiti unavyoendelea na hatua zilizofikiwa hana majibu anakuambia anajua mtafiti wa nje kitu ambacho sio sawa katika taratibu za vibali vya kufanya tafiti za aina hizo’’ Alifafanua Dkt. Nungu.
Dkt. Nungu amesema haya na mambo mengine mengi ndiyo yaliyotufanya tukusanyike hapa kama wadau ili tuweze kufahamishana na kupeana ushauri wa namna ya kuboresha namna ya utendaj kazi kwenye eneo la utafiti ili ziweze kuleta tija nchini.
Kwa upande wake makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka ambaye ni mshirki wa warsha hiyo amesema utafiti unasaidia kutatua changamoto za nchi lakini pia lazima uzingatie vigezo na maadili ya kufanya taifi ili ulete tija kwa taifa.
Amesema ili Utafiti uingie na kutambuliwa na Taifa lazima upitie COSTECH ambao ndio waratibu wa tafiti zote ili kuweza kufikia malengo na serikali iweze kuutumia kwa manufaa ya jamii na Taifa badala ya watafiti kuishia kwenye taasisi zao kabla ya kushirikisha wadau.
Amesema kukutana kwao kwenye warsha hiyo kutasaidia sana wakuu wa taasisi kuweza kuwasaidia watafiti wake kutimiza vigenzo na masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za tafiti ili kuwa na Utafiti bora lakini pia kuwahisha kupata kibali kutoka COSTECH.
Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Lugano Kusiluka akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Mkutano katika Chuo Kiku cha Sokoine wakati wa Washa ya wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu na Taasisi za Utafiti wa Maendeleo.
ICGEB is Announcing for Postdoctoral Fellowships
International Centre for Genetic Engineering and Biotechnology ( ICGEB) is announcing the Arturo Falaschi Fellowships Programme: Postgradoctoral Fellowships.
The closing date for applicaiton is: 31st March and 30 September 2020. For more informaiton, please click here
Shortlisted Applicants in Second Round of Business Plan Innovation Challenge
Tanzania Digital Innovation Youth Empowerment Programme (TADIYE) is an innovation and entrepreneurship ecosystem development initiative, designed to inspire and promote technology-based young start up entrepreneurs in Tanzania. The project is funded by the Royal Danish Embassy in Tanzania and implemented through Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) in collaboration with two other key partners; Magilatech Company Limited and Institute for Management and Entrepreneurship Development (IMED)
For more information please clicks the link below In: