TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

Picha ya pamoja ya watumishi baadhi wa costech

NRF Yatembelea COSTECH 

 TAASISI ya Utafiti ya Taifa - Afrika Kusini (NRF) inayofadhili vigoda vya Utafiti vya O.R. Tambo  wametembelea Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) leo tarehe 20 Marchi, 2023  ili kujadili kuhusu Maendeleo ya Vigoda hivyo vya Utafiti toka vianze kutekelezwa nchini Tanzania. COSTECH ni msimamizi wa vigoda hivyo nchini Tanzania.

 Ugeni huo uliongozwa na Mkurugenzi wa Mitandao ya Maarifa na Mpango Mkakati wa Baraza la Utoaji wa Ruzuku za Sayansi (SGCI) na Ushirikiano wa Taasisi ya Utafiti wa Kitaifa (NRF) Afrika Kusini Dorothy Ngila aliyetoa wasilisho la muundo na kazi za NRF.

 Kwa upande wa COSTECH,Kaimu Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) Dkt. Beatrice Lyimo alitoa wasilisho la muundo na kazi za Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH.

 Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa COSTECH na ulifunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Bugwesa Katale.