COSTECH YAWATAKA WATAFITI KUJA NA MAANDIKO YANAYOJIBU CHANGAMOTO ZA MABADILIKO YA TABIANCHI
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt Amos Nungu na Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Elimu ya Juu na Utafiti Bi. Solbjorg Sjoveian toka Shirika la NORAD baina ya Serikali mbili (2) ya Norway na Tanzania.
Makubaliano hayo yamesainiwa kupitia hafla ya utiaji saini wa hati ya Makubaliano (MOU) wakati wa uzinduzi wa Programu ya Utafiti kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi iliyosimamiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe Dkt Sulaiman Jafo, tarehe 11 Oktoba 2023 - Ukumbi wa Mikutano, wilayani Kinondoni - Jijini Dar es salaam.
"Leo tulikuwa na ugeni hapa wa mabalozi toka Taifa la Norway na Swideni, tumesaini makubaliano na NORAD wanatoa billioni 9 ufadhili wa miaka 5 kupitia mfuko wa MTUSATE au maarufu kama NFAST kwaajili ya kufadhili Tafiti za mabadiliko ya Tabia nchi " amesema Dkt. Nungu
" COSTECH tunaratibu tafiti kupitia Mfuko wa MTUSATE ni kwaajili ya kufadhili watafiti wote toka Taasisi za Umma na Taasisi zisizo za umma , na Tabianchi ni mtambuka inaathiri binadamu au mimea kwenye ukame na njaa" alisisitiza
" Baada ya kusaini makubaliano haya, mkutano ujao tunategemea tutatoa hizi fedha ili timu za watafiti ziweze kuleta maandiko (proposals) yanayotatua changamoto za athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabianchi" Alihitimisha Dkt Nungu.
Aidha, Uzinduzi huo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe, Mwenyeti wa Bodi ya Kamisheni ya COSTECH, Prof Makenya A. Maboko, pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu toka WyEST, Prof ladislous Mnyone na watumishi wa Tume walishuhudia hafla hiyo.