TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY

SEKTA BINAFSI ZINAMCHANGO MKUBWA KUJENGA MIFUMO THABITI

Published at: Sat, Mar 4, 2023 3:39 PM

TUME ya Taifa ya Sayansi ya Teknolojia (COSTECH) imesema sekta binafsi
zinamchango mkubwa katika  kujenga mfumo thabiti wa kusimamia bunifu
Kitaifa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu wakati
akifungua msimu wa pili  wa  Vodacom accelerator  uliofanyika
katika Hoteli ya Hyatt_Kilimanjaro  iliopo  Jijini Dar es salaam.

Kutokana na hilo,Dkt. Nungu amesema,Serikali itaendelea kushirikiana
na sekta binafsi ili kuwezesha upatikanaji fursa za kidigitali ambazo
zitasaidia kujenga  mfumo jumuishi, shirikishi na endelevu kwa
maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini.

 "Leo tunao Vodacom accelerator na Smart Africa group walioamua kuja na
mpango jumuishi wa kuwezesha makampuni ya kibunifu machanga,
nawapongeza sana kwa hatua hii kubwa mliyofikia ,”amesema Dkt. Nungu.

Amefafanua kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kupitia COSTECH na
Benki ya CRDB kitasaidia upatikanaji wa fedha ambao utaziwezesha
bunifu nyingi kupata mitaji,ikiwemo kupata ushauri na maarifa ya
kuingiza bidhaa za kibinifu sokoni.

“Ushirikiano wa serikali na sekta binafsi,utasaidia kuongeza fursa kwa
vijana na wanawake ili kujiinua kiuchumi,ikiwemo kujiajiri wao
wenyewe,”amesema Dkt. Nungu.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali VODACOM, Nguvu
Kamando,alisema ubunifu ndio moyo wa Vodacom na kuahidi kuwa
wataendelea kuweka mazingira mazuri,kutoa vifaa pamoja na rasilimali
muhimu za kuchochea ukuzaji wa makampuni machanga ili yaweze kukua na
kubiasharishwa.

Naye Mbunifu na mwanzilishi wa Shule Yetu,toka atamizi ya DTBi iliyo
chini ya COSTECH, William Elia Mpuya,ambaye pia ametangazwa mshindi
miongoni mwa “Top Runners”amepongeza jitihada zinazochukuliwa na
Serikali pamoja na Sekta Binafsi.