Kusitisha Kwa Muda Huduma Za Kumbi Za Mikutano

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Inapenda  kuwatangazia wateja na wadau wake wote kuwa imesitisha kwa muda kutoa  huduma za kukodisha kumbi zake zote kuanzia tarehe 23 Machi, 2020 hadi  itakapotangazwa hapo baadaye. Hii ni kutokana na Mlipuko wa virusi vya  Korona.
Anna G. Ngoo

Kny: MKURUGENZI MKUU