Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Yatoa Mafunzo Kuhusu COSTECH kwa Wajumbe Wapya wa Bodi

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetoa mafunzo kwa Wajumbe wapya wa Bodi kuhusu  Tume (COSTECH). 

Mafunzo hayo yalitolewa hivi karibuni katika ukumbi mdogo wa COSTECH, yalifunguliwa na Mkurugegenzi wa COSTECH Dkt. Amos Nungu.

Dkt. Nungu aliwakaribisha wajumbe wapya wa Bodi na baadaye kuwakaribisha wakuu wa idara ili kuweza kuwapitisha kwa ufupi wajumbe hao wapya ili waweze kuelewa majukumu ya Tume kwa ujumla. 

Akielezea muhtasari wa COSTECH Kaimu Meneja Kitengo cha Huduma za Sheria Bw. Ernest Barulo alisema,  Shughuli   zaTume  ya  Taifaya  Sayansi  naTeknolojia  zilianzishwa  rasmimwaka  1972 chini  yaBaraza la ufafiti (Tanzania National Scientific Research Council)  kwa kifupiUTAFITI,  lakini  mwaka1988 lilibadilishwa  kuwa  Tumeya  Taifa ya  Sayansina Teknolojia  kwa  kifupi (COSTECH)  kwamujibu wa   sheria   Na.7ya bunge   ya mwaka  1986.

Bw. Barulo alisema majukumu   Makuu ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ni pamoja na kuishauri Serikali kuhusu mambo yote yanayohusu Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na matumizi yake katika maendeleo Kiuchumi na Kijamii nchini.

Aidha sekretariati inasimamia utendaji wake wa kila siku wa Tume, kwa kupitia kituo kimoja na kurugenzi tatu kama ifuatavyo: Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia (CDTT), Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP), Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa (DKM) na Kurugenzi ya Huduma za Jamii (DCS)

Kwa upande wa Kituo cha Kuendeleza na Kuhawilisha Teknolojia, Dk.Athman Mgumia alisema Kituo kinajishughulisha na masuala ya uhawilishaji wa teknolojia inayoibuka,maarifa ya ufundi kwa wazawa,utunzaji na usimamizi wa mazingira; miliki ya ubunifu,na tutoaji wa tuzo za sayansi na teknolojia.

Wakati Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uratibu na Uendelezaji wa Utafiti (DRCP) Dk Bugwesa Katale alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya kuratibu na kuhamasisha utafiti, kutoa vipaumbele vya utafiti na kushauri uwekezaji wa fedha za utafiti. 

Pia alisema huongoza Mfuko wa Taifa wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) kupitia kamati za ufundi za utafiti na Maendeleo katika kuandaa ajenda za utafiti.

Alifafanua kuwa COSTECH ina Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa chini ya kaimu Mkurugenzi Dkt. Philbert Luhunga ambaye yeye alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya Ukusanyaji, Uhifadhi, na Usambazaji wa taarifa za Sayansi, Teknolojiana na Ubunifu.

 Naye Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Jamii Anna Ngoo alisema Kurugenzi hii inashughulika na masuala ya Usimamizi wa Fedha,ukijumuisha, masuala ya Utumishi na Wafanyakazi, Utawala, Ruzuku ya Serikali na Ripoti za Wakaguzi.

Mkurugenzi Mkuu Dkt. Nungu alihitimisha kwa kuwashukuru Wajumbe wapya wa Bodi na kuwakaribisha COSTECH pamoja na kuwashukuru watoa mada wote kutoka katika

Kurugenzi za Tume.

EDITED
Picha ya pamoja ya Wajumbe wapya wa Bodi na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia mara baada ya kumaliza Mafunzo kuhusu COSTECH