Maonesho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu Yang'ara

Maonesho ya Sita (6) ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu yamefunguliwa rasmi Jumatano tarehe 28 Aprili, 2021 na mgeni rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Kaimu Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Dkt. Philbert Luhunga.

Akifungua maonesho hayo, Dkt. Luhunga, alisisitiza kwa upande wa Tume tunajivunia kuona jamii na hususani watafiti na wabunifu wetu wanawekeza muda wao na kuzitumia bunifu mbalimbali kwa kuonyesha matokeo ya tafiti mbalimbali ili kusaidia wananchi kuweza kubadilisha maisha yao kupitia Sayansi Teknolojia na Ubunifu (STU).

Kwa upande wa Rasi wa Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia- CoET, Prof Bakari N.N Mwinyiwiwa yeye aliwakaribisha  wageni mbalimbali waliotikia ushiriki wa maonesho hayo kwa kupongeza uwepo wa programu mpya za wakadiriaji wa majengo, wabunifu wa majengo pamoja na wapimaji wa ardhi kwa kuwashukuru idara zote zilizojitokezaka kushiriki maadhimisho hayo.

Aidha maonesho hayo yalijumuisha jumla ya ya washiriki 65 kuonesha matokeo ya tafiti mbalimbali kwa jamii kutoka kwa walimu na wanafunzi wa Uzamili pamoja na kundi la wanafunzi wa shahada ya kwanza (undergraduate) hususani kwa Ndaki ya Utafiti na Ubunifu- CoET, yanayoendelea kuadhimishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dkt. Luhunga alihitimisha kwa kuwapongeza waratibu kwa maandalizi mazuri kwa kuwakusanya wabunifu pamoja na kutumia nafasi hii kuwapa moyo wabunifu na kutoa rai kwa washiriki wote kuunga mkono kauli mbiu hii “Utafiti na ubunifu kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda na Jamii Tanzania” ili kuendana na kauli mbiu ya nchi yetukatika Viwanja vya Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (COET).


Picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Maonesho ya 6 ya  Wiki ya Utafiti na Ubunifu ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Dkt. P. Luhunga,  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maarifa (mwenye koti la  drafti) kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)  yaliyofanyika katika Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (COET) Chuo Kikuu  Dar es salaam (UDSM).