Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Washiriki Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi - 2021

Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia- COSTECH wameungana na wafanyakazi wenzao kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali kuadhimisha Kilele cha Siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) zinazofanyika uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa uliopo wilaya ya Temeke.
Maandamano kwa Mkoa wa Dar es salaam yameanzia Jengo la TUCTA viwanja vya mnazi mmoja na baadaye kuelekea katika viwanja vya Uhuru uwanja wa Taifa ambapo Taasisi mbalimbali za Serikali zimejitokeza zikiwa na mabango yaliyobeba ujumbe tofauti ambapo kwa mwaka huu 2021 kauli mbiu isemayo " Maslahi bora, Mishahara Juu na kazi iendelee".

Tume tunaahidi kuendelea kukuza Utafiti na Ubunifu ili matokeo ya Utafiti yaweze kutafsiriwa kwa vitendo kupitia matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) na kuunga mkono jitihada za kuyafikia maendeleo endelevu ya Taifa kwa ujumla.Picha ya pamoja ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kabla ya kuelekea katika Maandamano ya Sherehe za Mei Mosi Uwanja wa Uhuru  wilaya ya Temeke, Dar es salaam. Mei 1, 2021.Sehemu ya Maandamano ya maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)  watumishi wa Tume wakiungana na watumishi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali viwanja vya Uhuru.