COSTECH Yawakutanisha Watafiti na Wanahabari Kuandaa Vijarida vya Miradi ya Ubunifu (Project Brief)

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos M. Nungu amefungua warsha ya uandaaji wa vijarida vya matokeo ya utafiti na ubunifu (Research and Innovation Impact Bulletin) Septemba 27, 2021 kwa kuwakaribisha washiriki ambao ni watafiti na waandishi wa habari ili waweze kujenga hoja kwa pamoja, kushiriki katika uboreshaji wa maandiko hayo ya kitafiti na kupanga vizuri taarifa zitakazowasilishwa kwa utaratibu wa vijarida vya miradi ya utafiti (project brief).

Dkt.  Nungu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika kwa  siku tatu (3) kuanzia tarehe  27 hadi 29 Septemba, 2021 katika ukumbi  wa mikutano ulipo ndani ya Ofisi za Makao Makuu ya COSTECH, Dar es  salaam, ambapo amewashukuru watafiti na waandishi wa habari kwa kuitikia  wito na kusisitiza kutumia nafasi hii ili kuandaa maandiko  yatakayotumika na wasomaji wengi zaidi, kujenga hoja kwa pamoja,  kuhamasisisha matumizi ya matokeo ya tafiti kwa lugha rahisi  itakayoeleweka kwa Umma. 

Warsha  hiyo imehudhuriwa na washiriki a kutoka Taasisi za utafiti na maendeleo  pamoja na Vyombo vya habari, Warsha hiyo imejumuisha miradi tisa (9)  yenye tija zaidi iliyofadhiliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa  Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Picha ya pamoja Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu (wa pili kulia - mwenye tai nyeusi), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji na Uendelezaji wa tafiti, Dkt. Paul Ochan'ga (wa tatu kulia) na Meneja wa Sayansi ya Jamii, Hildagalda Mushi (wa kwanza KushotoWatafiti na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa warsha ya uandaaji wa vijarida vya matokeo ya utafiti na ubunifu, uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya COSTECH..

Mkurugenzi  Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos M.  Nungu amefungua warsha ya uandaaji wa vijarida vya matokeo ya utafiti na  ubunifu (Research and Innovation Impact Bulletin) Septemba 27, 2021 kwa  kuwakaribisha washiriki ambao ni watafiti na waandishi wa habari ili  waweze kujenga hoja kwa pamoja, kushiriki katika uboreshaji wa maandiko  hayo ya kitafiti na kupanga vizuri taarifa zitakazowasilishwa kwa  utaratibu wa vijaarida vya miradi ya utafiti (project brief). 

Dkt.  Nungu ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika kwa  siku tatu (3) kuanzia tarehe Septemba 27, 2021 mpaka Septemba 29, 2021  katika ukumbi wa mikutano ulipo ndani ya Ofisi za Makao Makuu ya  COSTECH, Dar es salaam, ambapo amewashukuru watafiti na waandishi wa  habari kwa kuitikia wito na kusisitiza kutumia nafasi hii ili kuandaa  maandiko yatakayotumika na wasomaji wengi zaidi, kujenga hoja kwa  pamoja, kuhamasisisha matumizi ya matokeo ya tafiti kwa lugha rahisi  itakayoeleweka kwa Umma. 

Warsha  hiyo imehudhuriwa na washiriki a kutoka Taasisi za utafiti na maendeleo  pamoja na Vyombo vya habari, Warsha hiyo imejumuisha miradi tisa (9)  yenye tija zaidi iliyofadhiliwa na Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa  Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) unaosimamiwa na COSTECH.