Tanzania Yang'ara kwa kutoa Washindi Watatu, Watangazwa Kupitia siku ya Kilele cha Maadhimisho ya OFAB

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia ilizundua rasmi jukwaa la teknolojia ya kilimo  maarufu kama “Open Forum on Agricultural Biotechnology ” (OFAB) kwa Tanzania mnamo mwaka 2009. Lengo mahususi la jukwaa la OFAB kwa Taifa la Tanzania ni kuwezesha ubadilishanaji wa maarifa (Knowledge-sharing) na kutanua wigo wa uelewa wa teknolojia ya Kilimo ambayo itachochea kuongeza ufahamu kwa kutambua mchango wa teknolojia ili kutengeneza mazingira wezeshi kwa watoa maamuzi. Jukwaa la OFAB Tanzania limekuwa likitengeneza uelewa wa masuala ya teknolojia ya kilimo kwa wadau kupitia njia za majadiliano ya pamoja, warsha, na semina na vikao n.k. Jukwaa limefanikiwa kuratibu mashauriano ya pamoja na Bunge, Mamlaka za Udhibiti ubora, watunga sera na watoa maamuzi, wakulima, watafiti na wanasayansi, chimbuko la tasnia husika na vyombo vya Habari kujadili  kuhusu amsuala yahusianayo na teknolojia ya kilimo kwa ujumla na hususani teknolojia ya kilimo. Vilevile, Jukwaa limeandaa ziara ya kuona-ni-kuamini (seeing is believing) kwa wadau kupita uwezeshaji wa vitendea kazi kwa ndani na nje ya Tanzania. Hatahivyo, Jukwaa la OFAB Tanzania liemekuwa likishirikisha jamii kupitia maenoesho na majadiliano ya mara kwa mara kupitia midahalo. Jukwaa la OFAB limekuwa likiendeshwa katika nchi kumi (10) ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Ethiopia, Msumbiji na Rwanda na kusimamiwa na Taasisi ya Teknolojia ya Kilimo ya Afrika (African Agricultural Technology Foundation – AATF).


PICHANI: Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Amos Nungu (aliyeketi pichani), Mshindi wa upande wa Redio, Bi. Hellen Isdory Kwavava (aliyesimama kushoto), mshindi upande wa machapisho (print media), Bi. Fatma Abdul (wapili kutoka kushoto) na mshindi upande wa Luninga/Televisheni, ndg. Mshana (hayupo pichani) na ndg. Calvin Gwabala (Wakwanza kulia) katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa ushindi wao uliofanyika kwa njia ya mtandao, Ofisi za Makao Makuu, COSTECH – Dar es salaam.

Jukwaa la OFAB limekuwa na utaratibu wa kuendesha Mkutano wa Mwaka kwa mataifa yote wanachama ili kutathimini tija ya utendaji kazi wa miradi na vilevile kusherekea mafanikio ya Jukwaa hilo. Kwa mwaka huu 2021 Jukwaa la OFAB limepanga kuadhimisha tukio la siku ya Kilele cha Mafanikio yaani “OFAB Day” siku ya Septemba 28, 2021. Tukio hilo litahudhuriwa na Vyombo vya Habari, waombaji wa ruzuku ya uandishi wa Habari, Wakuu wa Taasisi ambazo Jukwaa la OFAB husimamiwa, wajumbe wa kamati za programmu ya OFAB pamoja na wadau wengine. Mataifa yote kumi (10) yaendeshayo majukwaa ya OFAB yatashiriki katika mkutano huu muhimu utakaorushwa kwa njia ya mtandao. Washindi washindano la OFAB walitangazwa kupitia Mkutano wa siku ya hiyo. Maombi ya waombaji wa ruzuku ya uandishi wa habari ilifunguliwa kwa waansihi wote wa Habari kwa nchi zote kumi (10) na Tanzania kuwalishwa na washiriki watano (5) ambao ni waandishi wa Habari kwa kuwasilisha maombi yao kwenda Taasisi ya Teknolojia ya Kilimo ya Afrika (AATF) kwa kufanyiwa mapitio. 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH, Dkt. Amos Nungu aliwapongeza washindi kutoka makundi matatu kupitia kilele cha maadhimisho ya siku ya Jukwaa la OFAB, yaliyofanyika Septemba 28, 2021, washindi hao walipatikana kupitia Shindano la OFAB kutoka Mataifa washirika kumi (10). Washindi kutoka Taifa la Tanzania ni: -

1. Mshindi upande wa Redio - Bi. Hellen Isdory Kwavava.

2. Mshindi wa upande Luninga/Televisheni - ndg. Mshana na ndg. Calvin Gwabala.

3. Mshindi wa Upande - machapisho (print media)- Bi. Fatma Abdul.

Tuzo hizo zenye lengo la kuchagiza matumizi ya teknolojia ya kilimo kupitia uandishi wa Habari ili kuweka mazingira wezeshi kwa watoa maamuzi kwa kuongeza uelewa na tija katika sekta ya kilimo kwa ujumla

MWISHO